Mlinzi wa Zamani wa Leicester City Gerry Taggart amesema kuondoka kwa Jamie Vardy kwenda Arsenal kunaweza kuwa janga kwa Leicester.
Vardy ambaye jana alitegemewa kutoa tamko lake la kuhamia kwa washika Bunduki mpaka sasa hajasema chochote na ameambatana na kikosi cha England huko Ufaransa kwa ajili ya Euro za mwaka huu.
Kijana wa miaka 29 Jamie Vardy kutoka Leicister City anatarajiwa hii leo kutoa majibu iwapo atajiunga na Club ya Arsenal kabla hajaelekea kwenye michuano ya Euro za mwaka huu akiwa na timu ya taifa la Uingereza.Arsenal tayari wamefikia makubaliano na Leicester na wamemwekea mezani Vardy kitita cha fedha kwa miaka minne.
Vardy bado alikuwa anatafakari kama awaache Mbweha kuelekea kwa washika Bunduki. Itakumbukwa Vardy aliisaidia sana Leicister katika kutwaa taji la Ligi kuu akifunga mabao 24.
Post a Comment