0

Ajali mbaya ya gari imetokea kaskazini mwa Tanzania , ambapo basi aina ya Costa mali ya shule ya Lucky Vincent iliyoko eneo la kwa Mrombo ,limetumbukia katika mto Marera ulioko katika mlima Rhotia, , Karatu mkoani Arusha.

Mkasa huo umetokea takribani kilomita 25 kutoka katika geti la hifadhi ya taifa ya Ngorongoro ,takriban kilomita 150 kutoka mji wa Arusha.

Wanafunzi hao walikuwa wamesalia na kilomita 5 ili kufika sehemu waliokuwa wakielekea.

Taarifa za awali kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo akiwemo mwalimu ilisema kuwa basi hilo lilikuwa limebeba wanafunzi na waalimu wanaosadikiwa kuwa thelathini na tano.

Mwandishi wa BBC mjini Arusha Ally Shemdoe, aliyeko mkoani humo amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mvua kali inayoendelea kunyesha katika eneo hilo.

Anasema kwamba dereva alidaiwa kutoijua barabara hiyo hivyobasi alikosa mweleko na kuteleza kando ya barabara kabla ya kutumbukia korongoni katika mto Malera.

Wanafunzi na waalimu hao walikuwa safarini kuelekea Karatu kwenye shule ya Tumaini English Medium Junior Schools kufanya mtihani wa kanda wa majaribio ya kujipima uwezo kabla ya kufanya mtihani wa taifa wa darasa la saba wa Kanda.

Shule hizo mbili zimekuwa zikifanya utaratibu wao wa kawaida,

Taarifa kutoka katika hospitali ya Lutheran Karatu, kwa muujibu wa Mbunge Ester Mahawe aliyeko hospitalini hapo , ni kuwa maiti zilizopokelewa katika hospitali hiyo ni 32 hii ikiwa na maana , miongoni mwao waalimu wawili, dereva mmoja , na wanafunzi ishirini na tisa.

Kati ya wanafunzi waliopoteza maisha yao 10 ni wa kiume huku 18 wakiwa wasichana.

Aidha maiti zitahifadhiwa katika hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru.

Mkuu wa wilaya ya Arusha , Fabian Dagalo amewataka wananchi kuwa watulivu kutokana na tukio hilo baya, na kwamba serikali itatoa taarifa baadaye kuhusiana na msiba huo.

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post a Comment

 
Top