TP Mazembe imeweka rehani taji la Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kufungwa mabao 2-0 na wenyeji Wydad Casablanca katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora mjini Marrakech, Morocco usiku wa Jumamosi.
Mabao ya Wydad yamefungwa na Noussir Abdellatif dakika ya 44 na Reda Hajhouj dakika ya 66 kwa penalti.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu aliingia dakika ya 58 kuchukua nafasi ya Rainford Kalaba na akaipa misukosuko ya kutosha ngome ya Wydad.
Mazembe sasa inatakiwa kushinda 3-0 wiki ijayo nyumbani Lubumbashi.tetembelee Facebook Twitter Instagram kupitia LangMediatz. Com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment