0
Mkuu wa kitengo cha habari na Mawasiliano wa Yanha Jerry Muro.
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.MKUU wa kitengo cha habari na Mawasiliano wa Yanha Jerry Muro ameitwa kwenye kikao cha kamati ya maadili cha Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF kufuatia kitendo chake cha kupingana na kuishambulia katika kuelekea mechi yao ya Kimataifa ya kombe la Shirikisho Barani Afrika uliofanyika Juni 28.
 Hiyo inakuwa ni mara ya tatu kwa Muro kuitwa na anatakiwa kufika Julai 02 katika ofisi za TFF saa Nne asubuhi au kama atashindwa kufika basi atume mwakilishi wake au utetezi wake kwa njia ya maandishi.
Muro amethibitisha hilo na kusema kuwa amepokea barua hiyo na hii ikiwa ni mara ya tatu na katika mara zote amekuwa anashinda kwa hoja na kwa.wakati huu mkakati wao mkubwa kuona nafungiwa kujihusisha na masuala ya mpira na zaidi anashangaa ni jinsi gani wanasema amewashambulia kupitia vyombo vya habari.
Barua hiyo inamtaka Muro kujitokeza siku hiyo au hata kama hatoweza kufika basi atume utetezi wake kwa maandishi au mwakilishi wake na hata kama hatofika basi kikao cha kamati ya maadili kitaendelea kama kawaida na watatoa maamuzi kama kawaida.

Post a Comment

 
Top