’
Akiongea na mtangazaji wa Jembe FM, JJ, Wakazi amesema album yake inaweza kuwa tayari hadi kufikia mwezi ujao au August. Amesema nguvu zake nyingi zaidi zipo kwenye kuisuka album hiyo kwa sasa.
Miongoni mwa video ambazo zitakuja ni pamoja na ile ya ile ya Moyo, Sijutii na Party Exclusive. Pia anadhani kuwa single yake Kwanini aliyomshirikisha Barakah Da Prince inaweza kuitambulisha album hiyo.
Kwa upande mwingine Wakazi amedai kuwa kampuni yake ya Work Ethic inakuja kwa nguvu zaidi na kwamba anakuja na kitu kikubwa.
Amedai kuwa kampuni hiyo itakuwa ikisimamia pia vipaji vingine.
Post a Comment