Bodi ya Utalii Tanzania imetoa
taarifa kufafanua kuhusu Mlima Kilimanjaro baada ya shirika moja la
habari la Marekani kudaiwa kuchapisha taarifa iliyoonekana kuashiria
mlima huo unapatikana Kenya.
“Tungependa kusahihisha habari za kupotosha zilizochapishwa na Miami Herald, kwamba Mlima Kilimanjaro unapatikana Tanzania na si Kenya,” taarifa iliyotiwa saini na meneja mkurugenzi wa Bodi ya Utalii ilisema.
Bodi hiyo inasema imeliandikia barua gazeti hilo na kulitaka lichapishe sahihisho.
Post a Comment