Msanii Joh Makini ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya wa ‘Perfect Combo’ amefunguka na kusema muziki wa bongo fleva sasa unaelekea sehemu nzuri na wale wote waliokuwa wanafanya ujanja ujanja kwenye muziki wataachwa kwani wakati umebadilika sasa na watu wanataka kusikia muziki mzuri na si ujanja ujanja.
Joh Makini aliyasema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio na kudai muziki wa bongo fleva sasa unajivua magamba kama nyoka na kuacha makapi na kwenda na watu wanaojua muziki kweli.
“Muziki wa bongo fleva kwa sasa naona ni kama kitu kinachokwenda huku kinajivua magamba, tulikotoka yaani zamani tulikuwa tunatengeneza Audio tu na zinafanya vizuri, baadaye zikaja videos ikawa mtu akifanya Audio ya kawaida akipiga na video kwa Adam Juma basi anatoboa kwenye muziki lakini baadaye wasanii wengi wakaanza kuzimudu gharama za Adam Juma hivyo ikawa lazima uwe na Audio kali ili ukipiga na Video kwa Adam Juma ngoma isogee.
Lakini watu wakavuka mipaka wakawa wanapiga video kali ingawa walikuwa wachache hivyo nyimbo zao zilipenya kutokana na video zao, imefika hatua saizi watu wengi wanaweza kumudu gharama za kufanya video nje ya nchi na kupiga video kali na wanatengeneza muziki mzuri” alisema Joh Makini
Kutokana na hali ya wasanii wengi kuweza kufanya video kali hata nje ya nchi Joh Makini anasema watu sasa hivi hawaangalia saana video bali wanataka kusiki muziki mzuri kuanzia kwenye Audio, mpka video na si kutegema video tu ili utoboe kama zamani.
“Hivyo basi package yote hiyo lazima iwe full kuanzia kwenye Audio mpaka Video, lakini muziki lazima uanze kwanza kuwa mzuri kwani saizi watu hawashangaa sana video sababu wanarudisha masikio yao kwenye muziki mzuri, mwisho wa siku haya yote yanaanzia kwenye muziki yaani studio. Nachoweza kusema turudi kwenye muziki saizi hakuna ujanja ujanja tena” alisema Joh Makini
eatv.tv
Post a Comment