0

Ruby amedai ameumizwa na kitendo cha Yamoto Band kushoot video ya wimbo wa SU bila ya yeye kuwepo.
Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio kuwa siku ambayo Yamoto Band walikuwa wakishoot video hiyo yeye alikuwa na mambo yake mengine hivyo alikuwa busy, lakini aliwaomba kama wanaweza wasubiri kidogo amalize na hizo kazi zake lakini wao waliamua kuifanya hivyo hivyo.
“Nimeumia sana maana audio ile tumefanya muda mrefu na waliweza kusubiri mpaka tukakamilisha iweje kwenye video washindwe kunisubiri, maana hii kazi tunasaidiana,” alisema Ruby.
Hata hivyo meneja wa kundi hilo la Yamoto Band, Said Fella hivi karibuni akiongea kwenye kipindi cha E News cha EATV alidai kuwa Ruby aliwaeleza kuwa alikuwa ana ‘stress’ ndio maana alishindwa kutokea kwenye video ya wimbo.

Post a Comment

 
Top