0




Beki wa zamani wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza Gary Neville amefutwa kazi na klabu ya Valencia ya Uhispania baada ya kuhudumu kama meneja wao kwa chini ya miezi minne.
Mkufunzi huyo wa umri wa miaka 41, ambaye yumo kwenye benchi la kiufundi la Uingereza, alipewa kazi Desemba.
Valencia walishinda mechi tatu pekee kati ya 16 walizocheza ligini chini ya Neville, na mechi 10 kati ya 28 kwa jumla katika mashindano yote.
G NEVILLE
Neville amesema alitaka sana kukaa Valencia lakini matokeo hayakufikia kiwango chake na viwango vinavyohitajika na klabu hiyo.
Ameongeza kwamba anafahamu wazi kwamba “tumo katika biashara ya kuangalia matokeo”.
Ndugu yake mdogo, Phil, amekuwa kwenye benchi ya kiufundi Valencia na ataendelea na kazi yake.
Neville alianza kutakiwa ajiuzulu baada ya klabu hiyo kucharazwa 7-0 na Barcelona mechi ya kwanza ya nusu Copa del Rey mwezi Februari.



Post a Comment

 
Top