Rais Dr john Pombe magufuli akiutubia |
Rais MAGUFULI amesema hayo wakati akizungumza na wananchi katika uwanja wa shule ya sekondari ya CHATO mara baada ya kuwasili nyumbani kwake katika kijiji cha MLIMANI, Mkoani GEITA ikiwa ni mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa Rais.
Aidha ametoa wito kwa kila mtanzania kufanyakazi kwa juhudi ili nchi iondokane na utegemezi wa misaada ya wafadhili ambayo huambatana na masharti.
Amesema jukumu kubwa lililo mbele ya watanzania kwa sasa, ni kushikamana na kujisimamia katika maendeleo ili kila mmoja ahakikishe anaongeza uzalishaji na utendaji kazi mahali pake pa kazi.
Kuhusu tatizo la wafanyakazi hewa, Rais MAGUFULI amesema matarajio ni kuwa uhakiki unaofanywa nchi nzima utaisaidia serikali kubaini wafanyakazi hewa wengi zaidi na kunusuru fedha nyingi zaidi za watanzania.
Post a Comment