Maharamia saba kutoka Somalia
wamefungwa jela na mahakama nchini Ufaransa baada ya kupatikana na
makosa ya kuteka boti na kuua mmiliki wake mwaka 2011.
Waliteka boti la Christian na Evelyne Colombo kwenye Ghuba ya Aden.
Wawili hao walikuwa kwenye safari ya kutalii dunia.
Christian aliuawa na mwili wake kutupwa baharini, naye mkewe akashikiliwa mateka kwa saa 48 kabla ya kuokolewa na wanajeshi wa Uhispania.
Maharamia wawili waliotambuliwa kama Farhan Abdisalamn Hassan na Ahmed Abdullahi Akid, na ambao walidaiwa kuhusika katika kuwatafuta na kuwapa kazi maharamia, walifungwa jela miaka 15.
Farhan Mohamoud Abchir, aliyekuwa hajatimiza umwi wa miaka 18 wakati huo na ambaye alianza kuugua ugonjwa wa kuchanganyikiwa kiakili akiwa gerezani kwa mujibu wa wakili wake, amepewa kifungo cha miaka sita jela.
Mwendesha mashtaka alikuwa amependekeza wafungwe miaka 22.
Post a Comment