Baada ya gumzo aliloliacha Lady jaydee kuhusu show yake ya masaa matatu mfululizo kuwa hakuna msanii mwengine wa kike ambaye anaweza kufanya hivyo, Ruby amefunguka na kutetea uwezo wao.
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, amesema kuperform show kama hizo na live band ni kitu cha kawaida kwa msanii.
“Kuperfom masaa matatu ni kitu cha kawaida kwa msanii ambaye yupo serious na kazi, hauko serious usijiite wewe msanii, msanii unatakiwa uwe perfect every where, fanya mazoezi usijifanye kwamba hujui, fanya mazoezi utaweza kuperfom zaidi ya masaa matatu”, alisema Ruby.
Pia Ruby amesema yeye binafsi anaweza kufanya show kama hiyo ya masaa matatu hata na zaidi, kwani kwake ni kama anafanya mazoezi tu.
“Mi naweza kuperfom masaa matatu kwa sababu nimekuwa nafanya hivyo kabla sijaingia kwenye bongo fleva nimeanza kuimba live kanisani, tunaperfom zaidi ya masaa matatu na masaa matatu kwangu ni kama kufanya mazoezi”, alisema Ruby.
Post a Comment