0
KOCHA Zinedine Zidane amesema nyota wake, Cristiano Ronaldo yuko fiti kwa asilimia 100 kwa ajili ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini amekiri Mreno huyo atalazimika kucheza na maumivu ili kumaliza mechi hiyo
.
Mfaransa huy na mchezaji wa zamani wa Real Madrid amesema hakuna wasiwasi Ronaldo ataanza dhidi ya mahasimu wao, Atletico Madrid na anatarajia atamalaiza mechi.
 
Ronaldo aliumia Jumanne baada ya kugongana na Kiko Casilla kwenye mazoezi na akalazimika kutoka nje kutubiwa na nesi mguu wake.


Zidane alisema maneno kama hayo kabla ya mchezo wa Nusu Fainali ya michuano hiyo dhidi ya Manchester City Uwanja wa Etihad mwezi April, baada ya Ronaldo kuumia nyama.

Lakini Mfaransa huyo alisistiza jana: 
"Si kitu kile kile. Alikuwa anasikia maumivu makali, lakini kwa sasa yupo fiti kwa asilimia 100, na zaidi ya hayo anacheza fainali. 
"Unapocheza fainali kama unasikia maumivu yoyote, unajipa ujasiri wa kuahau. Alikuwa anasikia maumivu kidogo, lakini si kitu na kesho (leo) atakuwa fiti kwa asilimia 100," amesema.

Post a Comment

 
Top