Amedai kuwa jinsi nguo zake zinavyofanya vizuri kwa sasa kumemfanya awe na mipango mikubwa zaidi siku za usoni.
“Kwa muda mfupi African Boy imenipa pesa ambayo naweza kusema kwamba imenisaidia vitu vingi sana. Ni kitu ambacho kinafanya vizuri sana, nikileta mzigo sasa hivi in two weeks au one week hata ukiwa mkubwa vipi, mara nyingi sana nakuwa nimemaliza,” Jux ameiambia lang Media tz.
Anasema mpango wake ni kuwa na duka kubwa litakalokuwa likiuza bidhaa zake tu. Kwa upande wa viatu vya brand yake, amedai kuwa aliletewa sample lakini hakuridhishwa na kiwango chake kwakuwa vitakuwa vikiuzwa kwa bei kubwa kidogo.
Amesema kiatu chake kitauzwa kwa shilingi laki mbili na kwamba kitakuwa na ubora wa hali ya juu.
Duka lako liko WAP
ReplyDelete