0


Usanii unaweza ukawa ni mgumu mno kwakuwa wakati mwingine wasanii hujikuta wakifanya vitu ambavyo hawakutarajia kuvifanya kwa kuwaambia mashabiki wao vitu vya uongo. 

Ndoa

Hivi karibuni mastaa wa Bongo na wale wa Kenya wameonekana kutumia style ya kuweka mitandaoni picha zinazowaonyesha wakiwa wanafunga ndoa na kuandika maneno yanayowashtua mashabiki wao wakati picha hizo zikiwa za location wakati wanatengeneza video zao.

Msanii wa kwanza kumwangalia ni Linex. Picha zake zilionekana mtandaoni mapema mwezi Januari mwaka huu.

Linex

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Linex aliandika, “Kuna maamuzi hayahitaji matangazo.” “Silence speaks volumes,” aliandika Linex kwenye picha nyingine. Baada ya picha hizo za kuwashtua mashabiki msanii huyo aliachia video yake mpya ‘Kwa Hela’.
Naye msanii kutoka TMK Wanaume Family, Chege alitembelea kiki hiyo mwezi Julai mwaka huu kwa kuweka mitandaoni picha za msanii mwenzake wa kundi hilo Temba akiwa kanisani anafunga ndoa. Picha hizo ziliwatoa povu mashabiki wa muziki huku wengi wakiwa wanafahamu fika kuwa msanii huyo tayari alishafunga ndoa siku nyingi.

Temba

“Naomba sana nisaidieni kumpa hongera Amani James kwa jambo hili la kheri HONGERA sana bro Temba,” aliandika Chege kwenye moja ya picha alizoweka kwenye mtandao wake wa Instagram.
Presha ya mashabiki ilishuka mapema mwezi Agosti mwaka huu baada ya msanii huyo kuachia video yake mpya ‘Wacha Waoane’ aliyomshirikisha Diamond na baadhi ya vipande vya video hiyo vikimuonyesha Temba akiwa anafunga ndoa.


Kwa upande wa Kenya alianza Jaguar mwishoni mwa mwaka 2014 alipost kwenye mitandao picha akionekana yupo kanisani akifunga ndoa na kuzua maswali mengi kwa mashabiki wa muziki lakini baada ya muda aliachia video yake ya ‘One Centimeter’ iliyoonekana kuwa na picha hizo zilizoonekana mwanzo mitandaoni.
jagur_weddo
Mshituko mkubwa uliibuka baada ya mapema mwezi Julai mwaka huu Akothee kupost picha mitandaoni akionekana akifurahia baada ya kufunga ndoa akiwa ndani ya shela.
13531968_1101664066571243_1094846367_n-1-2
“I am that woman who goes for what I wants & not what’s available, it’s my black beauty that caught his mouth Zero , irrespective of the no of children I have , he has taken me wholesale & I have welcomed him in my family , live once & live like‪#‎madamboss for richer for richest , my bed is warm now (you the papa of my pikin ) he is my King & am his queen in our small queendom!,” aliandika Akothee kwenye moja ya picha hizo.
Aidha msanii huyo alijitapa kwenye kipande cha video aliyopost kwenye Instagram akisema, “#madamboss , no apologies yes I do, honey are you coming with me to #luofestival “YES I DO .” Baada ya siku chache akaachia video yake mpya ‘Yuko Moyoni’.
Wiki hii picha za msanii mwingine wa nchi hiyo, Bahati zimeonekana kuenea mitandaoni huku baadhi ya watu wakijua kuwa amefunga ndoa na kumtakia Baraka zote ndani ya ndoa hiyo.
baha
“I told you I got it , u did chini ya Maji now we all know – let’s all celebrate @bahatikenya – Finally ameoa,” aliandika Dj Mo kutoka Kenya kwenye mtandao wake wa Instagram.
Hata hivyo imedaiwa kuwa picha hizo za Bahati ambaye mwezi Machi mwaka huu alitangaza kuwa anamzimia sana msanii wa filamu kutoka Bongo, Lulu ni picha za location akishoot video yake mpya ‘Mapenzi’ ambayo inatarajiwa kutoka hivi karibuni.
Swali ni je stunt hizi za ndoa zinakiki kweli?

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top