Baada ya lile drama kati ya star wa Bongo movie, Niva Supermariyo, na rapper Nay wa Mitego kushika moto kutokana na wimbo wa 'Shika adabu yako' alio uimba Nay na Niva kuamua kumjibu kupitia filamu ambayo aliipa jina la 'Maisha ya mtoto wa Manzese' sasa wameamua kuvaana live.
Wakizungumza na Enewz kwa wakati tofauti tofauti ili mastar hao waweke bayana tofauti zao lakini waliamua kutoleana uvivu kwa kupigana madongo ya live bila kukwepeshana.
Alipo ulizwa Niva kwanini aliamua kuingia kambi ili kuandaa filamu tu itakayo mponda Nay? Niva alisema “ Nay ni kama babaji kwahiyo hawezi shindana na mimi haniwezi kama yeye alizoea kuwaonea wanyonge mimi sasa haniwezi ,kimaisha kwanza hajanifikia na mtu mwenye akili huwezi kujianika sana vitu vyako vya ndani kama yeye anajiona star, kwanini anakimbiwa na wanawake”.
Enewz haikuishia kufanya mahojiano na Niva, Ilimlazimu kumtafuta Rapper Nay Wamitego kujua nini mtazamo wake kuhusu maneno ya Niva. Nay Wamitego alifunguka maisha anayo ishi Niva pamoja na gari alilopewa na Muhindi.
“ Kwa sehemu ambayo ninauhakika nayo kwa asilimia mia moja ni kwa Niva, Niva hana geto ana gari na alipewaga na Muhindi, alipeleka muvi namfahamu vizuri, Mimi natokea mtaani naimba sifanyi movie kwahiyo siishi maisha ya kuigiza”. Alisema Nay.
Aidha Niva ametoa sababu ya kutokuwepo sokoni kwa movie hiyo hadi sasa ni kutokana na kuzuiwa na uongozi wake baada ya kuona haina maana kutengeneza filamu kwa lengo la kujibishana na mtu kwakumwambia kuwa anaye anza anaweza asionekane mgomvi ila anaye malizia akaonekana kuwa ndio mgomvi. Lakini amesema kuwa Nay wa mitego akiendelea ataiachia tuu huku Nay akimtaka Niva kuonyesha mahali anapoishi kama alichoimbwa ni uongo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment