Najua wewe ni mmoja kati ya watu wanaojiuliza maswali nahodha wa timu ya taifa ya Sweden Zlatan Ibrahimovic
atacheza klabu gani msimu ujao, basi majibu yanakaribia kupatika hasa
baada ya Sky Sport kuripoti kuwa staa huyo yupo njiani kujiunga na klabu
ya Man United.
Sky Sport wameripoti kuwa Zlatan atakamilisha usajili wa kujiunga na Man United wakati wowote kuanzia sasa ila ni kabla ya michuano ya mataifa ya Ulaya kuanza, Sky Sport wanaeleza kuwa kocha wa Man United Jose Mourinho amepanga kusajili mshambuliaji mmoja katika dirisha hili la usajili ila Zlatan Ibrahimovic ndio chaguo lake.
Mtendaji mkuu wa Man United Ed Woodward na wawakilishi wa Zlatan wanaripotiwa kuwa katika mazungumzo ya mwisho ili kumsajili staa huyo kwa mkataba wa mwaka mmoja, Zlatan kwa sasa yupo na timu yake ya taifa ya Sweden anajiandaa mchezo wao wa kwanza wa Euro 2016 dhidi ya Ireland utakaochezwa June 13.
Post a Comment