Baadhi ya majaji katika mashindano hayo. |
Wanafunzi wa chuo cha
uandishi wa habari na utangazaji arusha (AJTC) Wanaendelea na mashindano ya
utangazaji katika chuo hicho ambapo kesho
yata tangazwa madarasa matano yatakayoingia fainali na hatimaye siku ya
ijumaa kujulikana mshindi.
Makamu mkuu wa chuo hicho Bw.Elifuraha Samboto
amewaasa wanafunzi wasishindane kwa ajili ya kupata fedha bali washindane kwa
lengo la kuinua vipaji vyao.
Aidha ameongeza kuwa
ili kuweza kupata ushindi ni lazima kila darasa washirikiane na wawakilishi wao kwa pamoja ili waweze
kupata ushindi.
Hata hivyo mshindi wa
kwanza atapewa shillingi laki moja na nusu na kombe lenye dhamani ya shilling
laki moja na nusu huku mshindi wa pili akipewa laki moja na mshindi wa tatu
atajinyakulia shillingi elfu sabini na tano.
Post a Comment