Baadhi ya wanafunzi wa ajtc wakitokaka nje ya ukumbi huo mara baada ya mashindano kuhitimishwa kwa siku ya leo.ambapo yataendelea tena siku ya kesho |
Mashindano ya kuwatafuta watangazaji bora katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha yameingia ungwe ya pili hii leo kwa madarsa mbalimbali kuwasilisha vipindi vyao
Bw. Elfuraha Samboto amesema
kuwa dhana ya mashindano hayo ni kuhakikisha
kuwa wanafunzi wanafunzi wanafanya mazoezi ya vitendo na kuwajenga
lakini pia kuwasaidia katika kupambana
na soko la ajira.
Makamu mkuu wa chuo cha AJTC Bw Elfuraha samboto kushoto akiwa na moja ya jaji katika mashindano hayo Bw Stephen Mlaki kulia |
Aidha
amewaomba wanafunzi kuonyesha ushirikiano kwa kila mmoja ambaye ataingia studio
kwa ajili ya kuwasilisha darasa husika asiachwe kana kwamba yeye ndiye
mshiindani peke yake.
Mashindano
hayo ambayo ni ya tisa
kufanyika tangu kuanzishwa
kwa chuo hicho, yamewapa wanafuni mwamko
wa kujifunza kwa vitendo jambo ambalo huwapelekea wao kukomaa na kuwa wazoefu katika fani.
Baadhi ya
wanafunzi katika chuo hicho wametoa pongezi kwa wakufunzi wao kutokana na suala
zima la kuandaliwa kwa mashindano hayo kwani yanawapa changamoto katika ushindani jambo ambalo huwafanya wao
kujiandaa kisaikolojia jinsi ya kufanya
kazi pindi watakavyoajiriwa.
Post a Comment